Nafasi za Kazi 200 za Madereva wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka (BRT)
Mofat Company Limited
Tanzania · Dar es SalaamFull-timeOn-site
Posted: 8 hours ago
Expires: Oct 9, 2026
Salary:
Not listed
Job description
Nafasi: Dereva wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka (BRT)Idadi ya Nafasi: 200Daraja la Mshahara: Grade 4Uzoefu: Angalau Miaka 3Mwisho wa Kutuma Maombi: 9 Oktoba 2026 MUHTASARI WA KAZI Dereva wa Basi la Mwendokasi (BRT) atawajibika kuendesha basi la mwendokasi kwa usalama, umakini na weledi, kwa kuzingatia ratiba, njia na vituo vilivyopangwa. Pia atahakikisha usalama wa abiria, kufanya ukaguzi wa basi, kuzingatia sheria za barabarani na taratibu za BRT, pamoja na kutoa huduma bora kwa abiria. SIFA ZA MWOMBAJI Muombaji anatakiwa kuwa na: Elimu ya Msingi, Kidato cha Nne (IV) na Kidato cha Sita (VI). Leseni ya Udereva Daraja C Plain iliyohakikiwa na Jeshi la Polisi. Cheti cha PSV kutoka VETA au NIT. Cheti cha BRT kutoka NIT. Uzoefu wa kazi wa angalau miaka 3 katika udereva wa magari ya abiria au mabasi. MAJUKUMU YA KAZI Kuendesha basi la mwendokasi kwa usalama, umakini na kuzingatia ratiba na vituo vilivyopangwa. Kuhakikisha usalama wa abiria, watumiaji wengine wa barabara na mali wakati wote wa safari. Kufanya ukaguzi wa basi kabla na baada ya safari ili kuhakikisha liko katika hali nzuri na salama kwa matumizi. Kuripoti mara moja hitilafu za kiufundi, ajali, matukio au changamoto nyingine zinazojitokeza wakati wa safari kwa msimamizi husika. Kuhakikisha basi linatunzwa, linakuwa safi na katika hali nzuri wakati wote wa matumizi. Kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani, taratibu za BRT na miongozo ya kampuni. Kutoa huduma bora kwa abiria kwa heshima, staha na weledi. Kufuatilia muda wa mwisho wa uhalali wa nyaraka za dereva na kutoa taarifa kwa wakati kabla ya nyaraka hizo kuisha muda wake. Kuhifadhi na kuwasilisha kwa usahihi taarifa za safari, matumizi ya nishati ya gesi na taarifa nyingine muhimu za uendeshaji wa basi. Kutoa msaada na kufuata taratibu za usalama wakati wa dharura, ajali au matukio mengine yasiyotarajiwa. Kuwa makini zaidi katika maeneo yenye vivuko vya waenda kwa miguu (zebra), vituo vya BRT na maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu. Kushirikiana na wasimamizi, waendeshaji wenzake na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha huduma ya usafiri inatolewa kwa ufanisi na kwa usalama. DARAJA LA MSHAHARA Grade 4 Mwisho wa Kutuma Maombi: 9 Oktoba 2026
The Grants Specialist is directly responsible for the administration of all aspects of publicly funded awards from pre-award to award implementation and closeout. Their duties incl...
See your job match
Sign in and add your CV/profile to see your match percentage.