# Nafasi za Internship Kaliman Electric Company – Operations Intern , Dar es salaam July 2026

Canonical URL: https://primejobalerts.com/jobs/nafasi-za-internship-kaliman-electric-company-operations-intern-dar-es-salaam-july-2026

Company: Kaliman Electric Company

Category: Manufacturing, Transport & Logistics

Location: Tanzania, Dar es salaam

Work type: Full-time

Work arrangement: On-site

Published: 2026-07-09

Expires: 2026-09-12

## Job Description

### Nafasi za Internship Kaliman Electric Company – Operations Intern

Kaliman Electric Company inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa wahitimu au wanafunzi wanaohitaji kufanya mafunzo kwa vitendo (Internship) katika nafasi ya Operations Intern. Huu ni mwaliko kwa vijana wachapokazi na wenye nia ya kujifunza na kukua kitaaluma katika sekta ya nishati na uendeshaji.

### Muhtasari wa Nafasi ya Kazi

- 
Jina la Nafasi: Operations Intern

- 
Mwajiri: Kaliman Electric Company

- 
Aina ya Kazi: Internship / Mafunzo kwa Vitendo

- 
Eneo la Kazi: Dar es Salaam, Tanzania

- 
Mwisho wa Kutuma Maombi: 15 Julai 2026

### Sifa na Vigezo vya Mwombaji

### Ili uweze kufikiriwa katika nafasi hii, mwombaji unapaswa kuwa na sifa zifuatazo

- 
Elimu: Awe na Shahada (Degree) au Stashahada (Diploma) katika fani ya Operations Management, Business Administration, Logistics, Supply Chain Management au fani nyingine inayofanana.

- 
Ujuzi wa Kompyuta: Awe na uwezo mzuri wa kutumia kompyuta, hususan programu za Microsoft Office (Word, Excel, na PowerPoint).

- 
Mawasiliano: Ujuzi mzuri wa mawasiliano ya mdomo na maandishi, pamoja na uwezo wa kushirikiana vyema na wafanyakazi wenzake (Team player).

- 
Nia ya Kukua: Awe mtu tayari kujifunza mambo mapya kwa haraka, kufanya kazi kwa kujituma, na mwenye nidhamu ya kazi.

### Jinsi ya Kutuma Maombi (How to Apply)

Kama unakidhi vigezo vilivyotajwa hapo juu, tafadhali tuma Wasifu wako (CV) pamoja na Barua ya Maombi kwenda kwa Idara ya Rasilimali Watu kupitia barua pepe ifuatayo:

Email: hr@kalimanelectric.co.tz

ANGALIZO: Hakikisha unataja jina la nafasi ya kazi (“Operations Intern”) kwenye kichwa cha habari cha barua pepe yako (Subject line).

### Mawasiliano na Maswali

### Kwa maelezo au maswali zaidi, unaweza kuwasiliana na mwajiri kupitia namba

Simu: 0652 594964

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Julai 2026.

Kaliman Electric Company — “GENUINE AND SAFE”

## Requirements

Apply by email: hr@kalimanelectric.co.tz

## Apply

Use the canonical Prime Job Alerts page for full application instructions and source verification.
