Nafasi 3 za kazi: Operations Manager – Lipa Airtel; Ihalula Company Limited, Sumbawanga, Rukwa Septemba 2026
Ihalula Company Limited
Job description
Operations Manager – Lipa Airtel
IHALULA COMPANY LIMITED inakaribisha waombaji wenye sifa kuomba nafasi ya Operations Manager – Lipa Airtel (Nafasi 3).
Majukumu Makuu
- Kusimamia shughuli zote za Lipa Airtel na kuhakikisha ufanisi wa operesheni.
- Kutathmini mwenendo wa mauzo na kuandaa ripoti za kila siku, wiki na mwezi.
- Kubuni na kutekeleza mikakati ya kuongeza wateja na miamala.
- Kuhudumia wateja na kutatua changamoto zinazohusiana na huduma za Lipa Airtel.
- Kushirikiana kwa karibu na Airtel katika utekelezaji na uboreshaji wa shughuli za Lipa Airtel.
- Kusimamia na kuhamasisha timu kufikia malengo yaliyowekwa.
Sifa za Mwombaji
- Awe na elimu ya Form Four na kuendelea.
- Awe na uzoefu katika Sales au Operations.
- Awe na uelewa wa Telecom na Airtel Money.
- Awe na uwezo mzuri wa uongozi na usimamizi wa timu.
- Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano, ufuatiliaji na utatuzi wa changamoto.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Tuma maombi yako kupitia
Email: recruitments@ihalulatraders.co.tz
Deadline
30 September 2026
Jiunge nasi katika kukuza na kuimarisha huduma za Lipa Airtel.